ZLATAN IBRAHIMOVIC AKANUSHA KUWA NA "TABIA MBAYA"

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amekanusha maoni yanayotolewa kuwa ni mtu mbaya, wakati alipokuwa kijiandaa kushuka dimbani leo kwenye Ligi Kuu England akiwa na umri wa miaka 34.

Msweden huyo ambaye alikamilisha uhamisho wake wa kutua United akitokea Paris Saint-Germain Juni mwaka huu aliiambia Sky Sports: “Watu wanasema mimi ni mtu mbaya, niko hivi mara vil, mimi ni mtu mzuri lakini ninapokuwa uwanjani ni simba.”

Aliongeza: “Siamini kuwa ni mwenye majivuno kama watu wanavyofikiria. Ninajiamini na binafsi ninaamini kuwa ni mwenye ujivuna.”


“Ninaamini ni suala langu binafsi katika ubinaadamu. Nina maono na ninalolifanyia kazi.”

No comments