STAA wa Manchester United, Adnan Januzaj anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Sunderland, amejipa matumaini ya kujing’arisha mwenyewe katika michuano ya Ligi Kuu England kwa kuisaidia timu hiyo kupata ushindi wa mfululizo katika michezo yake mbalimbali.

Msimu huu vijana hao wa David Moyes hawajaonja radha ya ushindi, ikiwa ni baada ya kushuhudiwa aliyekuwa kocha wao, Sam Allardyce akiondoka baada ya kupata kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya England muda mfupi kabla ya michuano hiyo kuanza.

Hata hivyo, Januzaj ambaye ameshaanza kuonyesha makali yake mapema akiwa na Sunderland, ana matumaini klabu yake hiyo mpya itapata ushindi wake wa kwanza hivi karibuni.

“Nimeshawahi kusema kuhusu malengo yangu ya kucheza soka na kuwaonyesha watu kile ambacho ninaweza kukifanya,” winga huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji aliiambia tovuti ya klabu hiyo.


“Ninachokiangalia ni wiki chache za mbeleni kwa sababu tumeshacheza na timu nyingi nzuri,” aliongeza nyota huyo.
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac