AISHA BUI SASA AJIONGEZA KWA KUGEUKIA UTAYARISHAJI

MSANII wa siku nyingi wa Bongomovies Aisha Bui amesema sasa ni wakati wake wa kugeukia kazi ya utayarishaji wa filamu kwa vile tayari ameshapata uzoefu wa kutosha.

Aisha alisema kuwa suala la kujiongeza ni la umuhimu katika kazi yoyote na kwamba sasa anataka kuwa mwigizaji na mtayarishaji huku pia akisambaza kazi zake mwenyewe.

Alisema katika ujio wake mpya baada ya kimya kirefu amefanikiwa kuanzisha kampuni yake ambayo ameipa jina la "Bad Girl" itakayokuwa ikisimamia kazi zake zote ikianzia kwenye filamu iitwayo "Mshale wa Kifo."


“Nina uzoefu mkubwa kwenye Bongomovies na najiamini ndiyo maana nimeanzisha kampuni kugeukia utayarishaji wa filamu na pia kusambaza kazi zangu mwenyewe," alisema.

No comments