ALEXIS SANCHEZ ADAI YUKO DARAJA MOJA NA MESSI, RONALDO

FULL kujiamini. Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez anajiamini kupita kiasi na amesema yuko katika daraja moja na mastaa wakubwa katika soka duniani kwa sasa, Lionel Messi wa FC Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.

Akikaririwa na gazeti la kila siku la Spain Sport, Sanchez alisema: “Nimefikia kiwango ambacho naweza kushindana na wachezaji mahiri, sijioni mnyonge kwa yeyote yule.”

“Ninalinganisha ubora wangu na Messi na Ronaldo. Nina uwezo sawa kama wao.”
Sanchez alijiunga na Arsenal akitokea Barcelona kwa ada ya uhamisho wa pauni mil 30 miaka miwili iliyopita na ameweza kuisaidia Arsenal kushinda makombe mawili ya FA na pia kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Premier League msimu uliopita.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile pia ameweza kuisaidia nchi yake kushinda Kombe la Copa America lililoisha hivi karibuni, ikiwa ni mafanikio ya kushinda Kombe hilo mara mbili mfululizo walipoifunga Argentina ya Lionel Messi kwa mikwaju ya penati.

Sanchez, 27, alikuwa nahodha wa Chile walipotoka suluhu Bolivia hivi karibuni.

Huo ukiwa ni mwendelezo wa matokeo mabaya kwa timu yao katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia.

Chile wameshinda mechi tatu katika mechi zao nne zilizopita na kufuzu na wako pointi mbili nyuma kutoka katika nafasi ya kufuzu kwenda Urusi (Kombe la Dunia).

No comments