ANDER HERRERA ATANGAZA VITA YA NAMBA KIKOSINI MANCHESTER UNITED

STAA Ander Herrera ni kama ametangaza vita baada ya kusema kuwa atapigania namba kwenye kikosi cha Manchester United na atakuwa tayari kujituma pindi kocha wake, Jose Mourinho atakapomuhitaji.

Msimu huu kiungo huyo amekuwa akipangwa mara chache katika michuano ya Ligi Kuu England tangu Agosti 14, mwaka huu wakati Manchester United iliposhinda mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth.

Staa huyo katikati ya wiki iliyopita alicheza dakika zote 90 ambazo walifungwa bao 1-0 na Feyenoord katika michuano ya Ligi ya Europa na jana alikuwa na matumaini ya kucheza muda wote dhidi ya Watford.

“Kitu pekee ambacho ninaweza kukisema, mimi ni mchezaji wa timu, nitakuwa tayari kuichezea pindi kocha atakaponihitaji,” Herrera alikiambia kituo cha MUTV.  

“Kwa ujumla kila mchezaji huwa anapenda kucheza tangu mwanzo kwa kila mechi lakini unapochezea timu kama hii jambo hilo si kazi rahisi,” aliongeza staa huyo.


Alisema atakuwa tyari kuichezea pindi kocha atakapomuhitaji na ndio maana anajifua vikali.

No comments