ANDREAS CHRISTENSEN ASEMA HATMA YAKE IKO MIKONONI MWA CHELSEA

STAA Andreas Christensen amekiri akisema kwamba kuhusu suala lake la kama atahamia moja kwa moja katika klabu ya Borussia Monchengladbach halipo mikononi mwake bali lipo kwa Chelsea ndio wanaoweza kuomba arejee Stanford Bridge au aendelee kubaki nchini Ujerumani.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Denmark alijiunga na miamba hao wa Ligi ya Gendesliga mwaka jana kwa mkopo wa muda wa mika miwili tangu kipindi hicho anaonekana kuwa tegemeo kwenye kikosi hicho cha Stadion im Borussia-Park.

Gladbich ina mpango wa kumsajili moja kwa moja beki huyo wa kati ifikapo mwisho mwa msimu huu lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 anasema kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Chelsea.

“Sifahamu kuhusu hatima yangu kama ipo mikononi mwa Chelsea ama Borussia Monchengladbach,’’ Christensen aliliambia gazeti la Rheinischen Post.

“Pengine uamuzi unaweza usiwe ni wa kwangu. Pia pengine naweza ni siwe na chagupo nba sitakuwa na la kufanya endapo Chelsea watanitaka nirejee kwao,” aliongeza staa huyo.


 Alisema kwamba itachukua muda mrefu kutokana na kwamba litakuwa jambo la kufikilia zaidi.

No comments