ANTOINE GRIEZMANN AWANIWA NA MSULULU WA KLABU KUBWA ENGLAND

KLABU kubwa za England zipo kwenye msululu wa kuwania saini ya mshambuliaji hatari wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann ambapo gazeti la Daily Star Sunday limesema kuwa thamani ya Mfaransa huyo inaweza kufikia pauni mil 80 mwakani.

Griezmann yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Manchester United, lakini wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa majirani zao, klabu ya Manchester City wanaoitaka pia huduma ya fowadi huyo.


Zaidi ya miamba hao wa jiji la Manchester, klabu nyingine mbili za London, Chelsea na Arsenal zinavizia kwa ukaribu dili hilo la kumnyakua Griezmann alieshinda tuzo ya ufungaji bora kwenye michuano ya Euro 2016.

No comments