ARSENE WENGER AIHURUMIA PSG KWA KUMWACHIA ZLATAN IBRAHIMOVIC

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ni kama anaihurumia klabu ya Paris Saint-Germain baada ya kusema kuwa ni kama imewapoteza wachezaji wengi kwa kumuachia nyota wake, Zlatan Ibrahimovic.

Ibrahimnovic aliondoka PSG akiwa na rekodi nzuri ya kuwa mfungaji bora katika kipindi ambacho aliipa mataji manne klabu hiyo ya Parc des Princes.

Baada ya kupata mafanikio hayo, nota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Sweden aliondoka na kwenda kujiunga na Manchester United akiwa mchezaji huru na PSG imeuanza msimu huu wa Ligi ya Ligue 1 kwa matokeo tofauti baada ya kushinda mechi mbili na hukuikipoteza moja kati ya nne.

Kutokana na hali hiyo, Wenger ambaye nae alikuwa akimtaka staa huyo atue arsenal, anasema kuwa licha ya PSG kubaki kuwa klabu kubwa chini ya kocha wao mpya Unai Emery, lakini anavyoamini wamempoteza kiongozi katika vyumba vya kubadilishia jezi.
Akizungumza juzi kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG, wenger aliema kuwa pamoja na kuwa timu hiyo itaendelea kuwa bora nchini Ufaransa, lakini imepoteza wachezaji wengi kwa kumuacha Ibrahimovic.

“Wataendelea kuwa timu kubwa Ufaransa, lakini wamepoteza wachezaji wengi akiwemo Ibrahimovic,” alisema Wenger.


“Ni kiongozi, nahodha na muhamasishaji ndani ya klabu na utapata shida utakapompoteza mchezaji kama huyu,” aliongeza kocha huyo.

No comments