ATLETICO MADRID YATHIBITISHA MAJERUHI TIAGO NJE WIKI MBILI

KLABU ya Atletico Madrid imesema kuwa inavyoonekana nyota wake Tiago anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili kutokana na majeraha ya misuri ya nyama za paja yanayomkabili.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 35 alitolewa nje ya uwanja na nafasi yake ikachukuliwa na Nico Gaitan dakika ya 61 ya mchezo wa Ligi ya mabigwa Ulaya ambao waliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya PSV.

Baada ya mchezo huo, Ateltico ilikwenda kumfanyia vipimo vya misuli na ndipo ikabainika ataweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wiki hizo mbili.


“Tiago alimaliza mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSV akiwa na matatizo. Baada ya kumaliza mchezo huo kesho yake kiungo huyo Mreno alifanyiwa kipimo cha MRI Scan katika hospitali ya Fremapde Majadahonda na ndipo tukabaini ukubwa wa tatizo,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo.

Ilieleza kuwa ripoti hiyo ya vipimo ilionyesha kuwa Tiago alipata majeraha kiasi ya misuli ya nyama za paja. 

No comments