AUDIO: “ASALI WA MOYO” KUTOKA KWA KATOTO MAYA WA AKUDO IMPACT
UNAPOITEMBELEA Akudo Impact utakubali kuwa wanastahili kuendelea kujiita Vijana wa Masauti kwa namna walivyo na waimbaji wenye sauti tamu.

Mmoja wa watu wanaoifanya Akudo iendelee kufanya vizuri kwenye idara ya uimbaji ni Katoto Maya.

Huyu ni mmoja wa waimbaji wazuri kabisa katika soko la muziki wa dansi hapa nyumbani na anadhihirisha hivyo kupitia wimbo wake binafsi “Asali wa Moyo” ambao tunakuwekea hapa uburudike nao.


“Asali wa Moyo” ni miongoni mwa silaha alizozitanguliza Katoto Maya katika mpango wake wa kuandaa albam itakayojulikana kama “One Day Yes”.

No comments