AUNT EZEKIEL SASA HATAKI TENA KIKI ZA SKENDO CHAFU

NYOTA wa filamu nchini, Aunt Ezekiel amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amebadilika na kuacha kiki za ajabu ajabu zikiwemo za kuvaa nguo fupi na badala yake anaangalia maisha ya familia.

“Nimekuwa mama naangalia vitu vya maana na upande mwingine, kesho na keshokutwa mwanangu atakua atakuta hayo matukio, oh mama yako alivaa kichupi, mama yako alikua hivi alikua vile ataiga nini mtoto kutoka kwangu?" Alioji.

Alisema kuwa kwa sasa anaangalia mara mbili ya pale alipokuwa mwanzo kwa lengo la kubadili mfumo wa maisha yake kama mtu mzima mwenye familia inayomtegemea.

Msanii huyo alikiri kwamba zamani alikuawa akivaa vibaya na kuwa na skendo mbalimbali kwa lengo la kutafuta kiki na kufahamika zaidi, lakini sasa hafanyi tena mambo hayo.


“Natambua kuwa nyuma yangu nina mtoto ambaye ananitegemea na anategemea malazi yangu, ndiyo maana nimeamua kuachana na mambo hayo.” Alisema Aunt Ezakiel. 

No comments