BALOTELLI ATABIRIWA MAKUBWA NA KOCHA WAKE WA NICE UFARANSA

KOCHA wa timu ya Nice, Lucien Favre amemtabiria makubwa straika wake Mario Balotelli baada ya kusema kuwa anavyoamini staa huyo atarejea kwenye ubaro wake baada ya kupitia mabao mawili mengine katika michuano ya Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1.

Wiki hii straika huyo Muitaliano alifunga mabao mawili ambayo yaliifanya Nice kuilaza Monaco kwa mabao 4-0 na hivyo kukwea kileleni mwa Ligi hiyo.

 Baada yua kuanza vibaya akiwa na Liverpool na alipokuwa akikipiga kwa mkopo katika klabu ya AC Milan, Balotelli hadi sasa ameshafunga mabao mawili katika mechi mbili alizoichezea Nice.

Kutokana na hali hiyo Favre anasema kuwa anavyodhani staa huyo mwenye umri wa miaka 26, kwa taratibu anaanza kufunguka.

“Mabao mawili aliyofunga na kufanya tuwe mbele kwa mabao 2-0, yalikuwa ni muhimu sana na kisaikolojia kwa ujumla yametujengea kujiamini. Tulifahamu tutashinda,” kocha huyo aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.


“Tukiwa na Mario tunafahamu bado tuna mengi ya kufanya ili tuweze kucheza kama timu,” aliongeza kocha huyo.

No comments