BARAKAH DA PRINCE ASEMA HANA KAWAIDA YA KUCHUNGUZA SIMU YA MPENZIWE

NYOTA wa muziki wa Kizazi Kipya, Barakah Da Prince, amesema kuwa hana kawaida ya kushika simu ya mpenzi wake Najma Dattan kwa lengo la kujua amewasiliana na nani.

Msanii huyo alisema kuwa hawezi kumuwekea mipaka mpenzi wake huyo na pia hajawahi kugusa simu yake na hata Najma hajawahi kushika simu yake Barakah na kwamba ndio utaratibu waliojiwekea.


Msanii huyo alikuwa akizungumzia sakata la Mr Blue ambaye aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi naNajma baada ya Mr Blue kulalamika kwamba Barakah na mchumba wake huyo wanataka kumuharibia ndoa yake.

No comments