BARNABA AWATAKA WASANII WENZAKE KUWEKEZA ZAIDI KWENYE AUDIO NA SI VIDEO

MSANII maarufu wa muziki wa Kizazi Kipya nchini ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki, Barnaba Classics amewataka wasanii wenzake kuwekeza nguvu nyingi kwenye kuandaa audio za nyimbo zao na si kuweka nguvu nyingi katikia uandaji wa video.


Msanii huyo alieleza kuwa hivi sasa baadhi ya wasanii wengi wamekuwa wakiweka nguvu nyingi katika uandaaji wa video na wengine kutia gharama kubwa katika kuhakikisha wanakidhi matakwa ya video hizo huku wakijisahau kuwekeza nguvu kwenye audio hali ambayo inashusha muziki nchini.

No comments