BATULI ASEMA BONGOMUVI HAIJAKUFA WALA KUSHUKA

 KIMWANA wa Bongomovies, Yobnesh Yusuf "Batuli" amepingana na kauli ambazo hutolewa na baadhi ya wasanii wenzake kuwa tasnia ya filamu imeshuka ama inaelekea kufa kabisa.

“Binafis siwezi kubishana na mtu kuhusu kusema kuwa Bongomovies imeshuka au imekufa, ni mtazamo wa mtu lakiniu kwangu naona ipo hai na watu wanaendelea kufanya kazi kama kawaida na watu wanapata riziki,” alisema Batuli.


Msanii huyo aliendelea: “Kwa kifupi Bongomovies haijafa na vyema watu kufanya utafiti na kuboresha sehemu zenye matatizo na sio kuwakatisha tamaa.” 

Alisema kuwa filamu bado zinalipa na kwamba msanii anapofanya biashara nyingine ni katika kujiongezea kipato kutokana na mfumo uliopo na sio kwa sababu Bongomovies imekufa.

No comments