BITCHUKA SASA KUREJEA JUKWAANI JUMAPILI HII DDC KARIAKOO


MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi Hassan Rehani Bitchuka wa Sikinde, sasa atarejea jukwaani Jumapili hii Septemba 25 ndani ya DDC Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Awali Bicthuka ilikuwa arejee Septemba 18, lakini akaamua kujiongezea wiki moja zaidi ya mapumziko.

Bitchuka aliyekuwa anasumbuliwa na jicho na kulazimika kufanyiwa upasuaji, ameithibitishia Saluti5 kuwa panapo majaaliwa Septemba 24 atakuwa DDC Kariakoo.

Mgeni rasmi wa onyesho hilo la Bitchuka kurejea jukwaani atakuwa ni Oscar Ndauka - mhariri kiongozi wa magazeti pendwa ya Global Publishers.

No comments