BRENDAN RODGERS ASEMA HAJAWAHI KUWA NA BIFU NA RAHEEM STERLING LIVERPOOL

KOCHA wa Brendan Rodgers amesema kwamba hajawahi kuwa na bifu na staa Raheem Sterling wakati akikipiga katika timu ya Liverpool.

Kauli ya kocha huyo imekuja baada ya wawili hao kufanya kazi pamoja kwenye klabu hiyo ya lakini Julai mwaka jana Sterling akawa wa kwanza kuondoka na kwenda kujiunga na Manchester City na kisha mwezi mmoja baadae Rodgers akafukuzwa.

Kabla ya kuamia Man City kwa ada ya pauni mil 44 kulikuwepo na taarifa zinazodai kwamba uhusiano kati ya Sterling na Rodgers haukuwa mzuri jambo ambalo raia huyo wa Ireland Kaskazini analikataa.


“Sikuwa na tatizo na Raheem,” alisema kocha huyo wa Celtic katika mahojiano na gazeti la Daily Mail.

No comments