CHAZ BABA ASEMA ASHA BARAKA NI MTAMBO WA KUZALISHA VIPAJI


JUMAMOSI usiku ndani ya Mango Garden Kinondoni, jijini Dar es Salaam, wakati Chaz Baba alipopanda jukwaa la Twanga Pepeta, alitamka sentensi moja ambayo ilitekenya hisia za wadau wa muziki.

Mwimbaji huyo wa Mashujaa Band ambaye kihistoria, ameng’ara zaidi na Twanga Pepeta, akamimina sifa kwa Asha Baraka.

Chaz Baba akasema: “Hongera sana mamaa Asha Baraka, wewe ni bingwa wa kuzalisha vipaji”.

Kwasasa Chaz yupo kwenye mgogoro wa kimkataba na Mashujaa Band na amekuwa akihusishwa sana na safari ya kurejea Twanga Pepeta.

No comments