CHOCKY NA KIMOBITEL WAKO MAFINGA, TWANGA WAKO MANGO GARDEN


WAKATI bendi ya Twanga Pepeta leo usiku itakuwa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam, mwanamuziki mwandamizi wa bendi hiyo Ally Chocky yeye atakuwa mjini Mafinga.

Chocky atakuwa Mafinga sambamba na mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta Hadija Kimobitel katika onyesho maalum litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Sigon Night Club na kupewa jina la "Usiku wa Ally Chocky".

Ally Chocky atapiga live nyimbo zake zote kali kwa kusindikizwa na bendi ya Sigon Band “Wazee wa Kipara”.

Akiongea na Saluti5, Chocky alisema bendi hiyo ya Mafinga tayari imeshazifanyia mazoezi nyimbo zote atakazozipiga na hivyo kila kitu kitakwenda vizuri bila mikwaruzo yoyote.

Waimbaji hao wawili Chocky na Kimobitel wameshawasili Mafinga tayari kwa onyesho hilo litakalofanyika leo. 

No comments