CHRIS BROWN AMPA MAKAVU MPENZIWE WA ZAMANI

BAADA ya taarifa kuwa anachunguzwa kwa kushindwa kumuhudumia mtoto, Chris Brown ameibuka na kumtolea mbovu mpenzi wake wa zamani mrembo Nia Guzman.

Awali ilielezwa kuwa Nia alimpeleka Chris kwenye vyombo vya sheria akimtaja kushindwa kupeleka fedha kwa ajili ya matumizi ya mtoto wao wa kike.


Akizungumza hayo ya mpenzi wake huyo wa zamani Brown alitumia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kuandika hivi: “Ni kama kila mtu anajua Nia ni nyoka mchimba madini na mtu asiye na kazi.”

No comments