MWANAMUZIKI Chiristian Bella amesema kuwa wimbo "Roho" alioshirikishwa na mkali Fid Q, umemuongezea mashabiki wengi wa muziki wa HipHop na wagumu.

Muimbasji huyo amekiri hilo wakati akiongea kwenye kipindi cha "Ngaz kwa Ngaz" cha EATV kinachoendeshwa na Salama Jabir.

“Leo kwenye Instagram natagiwa kila siku,” alisema Bella. “Watu wa hip hop wagumu hawapendagi hata tunapoimba utadhani kuna bifu au nini yaani, utasikia mzee umeuaa wale wagumu wale hawatakagi watu wa kuimba,” aliongeza.

Kwa upande wa Fid naye alikiri kuwa "Roho" imemsogeza zaidi kwa mashabiki wa kike.


“Kwa kifupi tumesaidiana sababu hata DM yangu imejaa warembo siku hizi wanakuja kuniuliza ‘Naomba Iyrics au nini’ yaani DM yangu imekuwa Lovely Kidogo,” alisema Fid.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac