Habari

CHRISTIAN ERIKSEN AJITIA ‘KITANZI’ TOTTENHAM

on

The Spurs playmaker poses with manager Mauricio Pochettino while signing a new contract
KIUNGO mchezeshaji Christian Eriksen ameamua kujitia kitanzi Tottenham kwa kusaini mkataba mpya wa miaka minne kwa wakali hao wa Premier League.
Nyota huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 24 aliwasili White Hart Lane akitokea Ajax mwaka 2013 na kuibuka kuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo ya kaskazini mwa London. 

TAKWIMU ZA ERIKSEN PREMIER LEAGUE

Mechi alizocheza: 101
Magoli: 23
Magoli aliyochangia: 23
Pasi: 5,047 
Akizungumza na Spurs TV, Eriksen alisema: “Kuna mipango mizuri ndani ya klabu hii na nisingesaini mkataba mpya kama nisingeliona hilo”
“Kuna kundi zuri sana, wachezaji waliojaa upendo  kwa kila mmoja, wafanyakazi wenye ushirikiano bora kwa wachezaji.”
Wote tuna tuna lengo moja tunalotaka kulifikia na nina matumaini tutafika tuendako.”
Christian Eriksen has committed his future to Tottenham by signing a new contract until 2020
Christian Eriksen akisaini mkataba mpya Tottenham 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *