CONTE ASEMA ANAHITAJI MUDA KUIBORESHA CHELSEA

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte anasema anahitaji muda kuiboresha timu yake ili kucheza anavyotaka yeye ili ipate matokeo bora.

The Blues kama wanavyoitwa walikwenda sare na Swansea City wakapoteaza mechi yao na Liverpool kabla kufanikiwa kuigonga Leicester City 4-2 kwenye mechi zao za hivi majuzi lakini ikaambulia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Chelsea.

“Ni kawaida wakati unaanza kwenye timu mpya unahitaji muda kutekeleza kile unachokusudia nami naamini tutaiboresha Chelsea,” Conte aliseama.


“Hii inamaanisha lazima tufanye kazi ya ziada timu nzima tuboreshe upande wa ulinzi wetu kwani iwapo unataka kuwa bingwa kisawasawa dawa ni kutofungwa mabao mengi hivyo.”       

No comments