CRAZY GK AMMIMINIA SIFA DOGO JANJA... aahidi kufanya nae kazi moja


MSANII mkongwe aliyewahi kufanya vizuri na kundi la East Coast Team, King Crazy GK amefunguka kwa kusema kuwa rapa Dogo Janja ndie msanii wake bora kwa sasa.

GK amesema anafurahishwa na jinsi rapa huyo anavyoweza kurapu akiwa ame-relax tofauti na wasanii wengine.

“Dogo Janja noma sana yule mtoto, wimbo wake mpya unaitwa “Kidebe”, ni rapa mkali angalia alichokifanya kwenye wimbo huo, anarapu akiwa flexible, yaani ana classic music,” GK aikiambia kipindi cha “Amplifaya” cha Clouds Fm.

Aliongeza: “Muziki ni kama ukishajua kuogelea, unaweza ukapiga mbizi, unaweza ukafanya chochote unachotaka. Mimi amenivutia sana na nitafanya nae kazi moja.”


GK kwa sasa anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo “Mzuri Pesa” ambayo aliiachia wiki mbili zilizopita.

No comments