DANNY DRINKWATER AIHAKIKISHIA UBINGWA LEICESTER KWA MARA YA PILI

KIUNGO wa Leicester City, Danny Drinkwater ni kama kaipa ubingwa timu yake baada ya kusema kuwa watakuwa wakifanya makosa kusema kwamba hawana ubavu wa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Vijana hao wa Claudio Ranieri leo watakuwa wakiiva klabu ya Club Brugge wakiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi baada ya msimu uliopita kutwaa ubingwa wa wa Ligi Kuu licha ya kuwa juzi waliamulia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Liverpool.

Hata hivyo, pamoja na kipigo hicho, Drinkwater anaamini kwamba Leicester City kwa sasa wameshajipanga kuhakikisha wanatwaa taji linguine.

“Hatukupenda iwe hivyo wakati tumeshaingia kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa,” alisema nyota huyo.


“Tunakwenda kuwaonyesha ni jinsi gani tulivyopanga kutwaa ubingwa huo,” aliongeza staa huyo.

No comments