DAR MUSICA YAIMARISHA UKUTA WAKE … 'mmiliki’ wa pili wa Ivory Band atimka


BENDI ya Dar Musica inayoongozwa na Jado Field Force imezidi kujiimarisha katika safu yake ya wapiga vyombo (ukuta) baada ya kumnyakua mpiga drum Sele Kadance kutuka Ivory Band.

Sele aliyeng'ara zaidi na Mashujaa Band, anakuwa ni mwanamuziki mmiliki wa pili kuondoka Ivory Band baada ya Jojoo Jumanne kurejea Twanga Pepeta mwezi uliopita.

Ivory Band iliyotokea ubavuni mwa Double M Plus, iliundwa kwa kumilikiwa na wanamuziki wenyewe wakiwemo Rama Petagon, Dogo Rama, Saleh Kupaza, Omary Kisila na hao wawili (Sele na Jojoo) waliotimka.

Dar Musica inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Ijumaa ya Septemba 16 ndani ya ukumbi wa Mango Garden huku ikiwa imesheheni wasanii kibao waliowahi kuitumikia Mashujaa Band kama vile waimbaji Raja Ladha, Jimmy, Jado mwenyewe, mpiga solo Proper, mpiga tumba Dulla Ngoma na mpiga drum Emma Chocolate.


Aidha, kiasi cha mwezi mmoja uliopita, Dar Musica pia ilimchukua mpiga kinanda wa Mashujaa Fred Manzaka.

No comments