DIEGO SIMEONE AMPIGIA NDOGONDOGO GRIEZMANN BALLON D'OR

KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone ni kama anampigia debe nyota wake Antoine Griezimann, baada ya kusema kuwa anastahili kuwania  tuzo ya mchejazi bora wa dunia, Ballon d’Or baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika kipindi cha miezi michache iliyopita.

Kauli ya kocha huyo imekuja baaada ya msimu huu Griezmann kuendeleza uchu wake kwa kuziona nyavu ambapo juzi aliipachikia timu yake mabao mawili na kuifanya iondoke na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Sporting Gijon 5-0 katika michuano ya Ligi Kuu Hispania La Liga.

Pamoja na nyota wengine wa timu hiyo kuziona nyavu, lakini alikuwa ni Mfaramsa Griezmann ambaye alitupiwa jicho na Simeone akisema kuwa anastahili kupambana na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika mbio za kuwania tuzo hiyo ya Ballon d’Or.

“Kwangu mimi mwaka jana Griezmann ndiye aliyekuwa mchezaji bora Ulaya,” alisema Simeone katika mkutano wake na waandishi wa habari mara baada ya mechi hiyo ya Jumamosi.

“Sina wasiwasi wowote na kile ninachokisema kutokana na kwamba alifika fainali zote mbli za Ligi ya Mabingwa na fainali Mataifa ya Ulaya "Euro 2016"  na alifunga mabao mengi katika mashindano hayo na La Liga. Ushiriki umemfanya kuwa na nguvu,” aliongeza kocha huyo.


Alisema kuwa ana natumaini anastahili kuwa miongoni mwa watakaowania tuzo hiyo ya Ballon d’Or kutokana na kwamba yuko katika ubora wa hali ya juu na kwamba ataendelea kuwa katika hali hiyo.

No comments