DIEGO SIMEONE APONGEZA KIKOSI CHAKE KWA SARE DHIDI YA BARCELONA

KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone ameonyesha kufurahishwa na matokeo ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya wapinzani wao Barcelona baada ya kupongeza uwezo wa kikosi chake katika mtanange huo.

Barca walikuwa wa kwanza kiliona lango la Atletico kupitia kwa bao la Ivan Rakitic, kabla ya Angel Correa kuwasawazishia wakali hao wa jijini Madrid.


“Katika kipindi cha kwanza tulilinda vizuri lakini hatukushambulia. Bao tulilolipata kipindi cha pili lilituamsha," alisema Simeone.

No comments