DK. CHENI ADAI RAIS MAGUFULI NDIYE ATAKAYEMALIZA TATIZO LA WIZI WA KAZI ZA WASANII

MSANII wa filamu nchini, Dk.Cheni amesema ana uhakika changamoto zinazowakabili wasanii likiwamo tatizo sugu la kuibiwa kazi zao linaweza kumalizika iwapo watatoa ushirikiano kwa serikali Rais Jonh Magufuli.

Aliutaja ushirikiano kwa wasanii kwa serikali kwamba ni kutaja vinara wote wanaojihusisha na hujuma hizo ili washughulikiwe kikamilifu kutokana na kile alichoelezea kuwa serikali imeonyesha nia ya dhati ya kumaliza tatizo hilo.


“Kwa muda mrefu tumekuwa hatufaidiki kwa kazi zetu tunazozifanya ila kwa selikali hii ya Magufuli na ufanisi wake hakuna shaka tutafikia malengo vizuri, kinachohitajika ni kutoa ushirikiano tu,” alisema.

No comments