Habari

DROGBA AWAPIGA DONGO ARSENAL, AWAAMBIA PAKA AKITOKA PANYA HUTAWALA

on

Didier Drogba scored 15 goals in 16 games versus Arsenal during his eight year spell at Chelsea
Didier Drogba hawezi kuinyanyasa tena Arsenal uwanjani , lakini amepata wasaa wa kuipiga dongo kwenye mtandano wa kijamii kupitia Theo Walcott.
Walcott ameendeleza mwanzo wake mzuri msimu huu kwa kufunga katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Chelsea na kuonyesha furaha yake kwa kupost picha yake ya ushindi kwenye Twitter.
Hata hivyo Drogba akajibu kwa kuandika: “Hongera kwa ushindi wenu @theowalcott, lakini ni rahisi panya kucheza pale paka anapokosekana.”
Drogba aliifunga Arsenal mara 15 katika michezo 16 aliyocheza dhidi ya timu hiyo kati ya mwaka 2004 na 2012.
Alifunga pia dhidi ya Arsenal wakati wa mechi za kujiandaa na msimu mpya huko America pale alipokuwa mmoja wa wachezaji waliounda  MLS All-Stars iliyofungwa 3-1.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *