Habari

DULLY SYKES ADAI SINGELI NI MUZIKI WA KIZARAMO

on

DULLY Sykes ameibuka na kusema
kuwa muziki wa Singeli ambao kwa sasa umeshika kasi, ni wa kabila la Wazaramo na
kudai kwa kabila hilo ndilo lenye asili ya muziki hapa nchini.
Alisema kuwa muziki wa Singeli unatokana na Mchiliku ambao ulikuwepo hapo zamani na ulikuwa wa ukipigwa Dar es
Salaam pamoja na Vanga, hivyo kuupa kibali ni muziki wa Kizaramo.
“Wazaramo ndio wenye miziki,
kwa sababu Man Fongo mwenyewe kama sio Mndengereko basi Mluguru na kama sio
Mluguru atakuwa Mzaramo au Mkwere, huyo Sholo Mwamba ndio haohao watoto wa kwetu, watoto wa Kizaramo” alisema. 
“Kwa hiyo Wazaramo ndio muziki wa kwetu ndio maana watoto kama
sisi hatushindwi kwenye muziki kwa sababu ndio jadi yetu,” aliongeza msanii huyo anayefanya poa hivi sasa na kibao “Inde”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *