EDINSON CAVAN AANZA KUVAA VIATU VYA IBRAHIMOVIC PSG

STAA Blaise Matuidi amesema kuwa mabao manne aliyofunga straika Edinson Cavani dhidi ya Caen, yanamfanya staa huyo wa timu ya Paris Saint-Germain kujiamini na kumfanya azidi kuzifumania nyavu.

Msimu huu staa huyo wa timu ya taifa ya Uruguay alikuwa akilaumiwa baada ya kushindwa kuvaa viatu vilivyoachwa na Zlatan, hata hivyo bao alilofunga katikati mwa wiki dhidi ya Arsenal katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na manne ya juzi aliyofungwa akiwa katika dimba la Stade Malherbe Caen yanaonekana kumfanya staa huyo aonekane kuanza kung’ara.

“Alikuwa ameshawatungua Arsenal na juzi akafunga manne dhidi ya Caen. Kwa hilo naweza kumpa tano na nina matumaini ataendelea kufanya hivyo,” alisema Matuidi.

“Sote tunafahamu Edi ni kijana ambaye anapaswa kujiamini. Sote tunalifahamu hilo lakini ni mchezaji mwenye kipaji na amekuwa akifunga mabao mengi kila msimu,” aliongeza staa huyo.


Alisema kwamba kwa ujumla wanamwamini nyota huyo na kwamba anachokifahamu ni kuwa msimu huu atafunga mabao mengi.

No comments