EL-HADJI DIOUF ASEMA STEVEN GERRARD NDIYE ALIYEMMALIZA MARIO BALOTELLI

STAA wa zamani wa Liverpool El-Hadji Diouf ameibua shituma nzito nzidi ya mkongwe wa klabu hiyo Steven Gerrard.

Kwa mujibu wa msenegali huyo, Gerrard alikuwa na wivu na hakuwa hakieshimu uwezo wa Balotelli.

“Gerrard ni mtu mwenye wivu ambaye hapendi watu wenye vipaji. Mario (Balotelli) ni mtu mzuri ambaye unaweza kumsikiliza. Sio mtu anayeweza kusababisha matatizo kwenye vyumba vya kubadilishia jezi.”

Diouf ambaye alifunga mabao matatu pekee kwa kipindi chote cha miaka mitatu akiwa Liver, amesema alimwambia Balotelli asitue Liver mwaka 2014.


“Nilimwambia asiende Liverpool. Haikuwa bahati yake mambo yasingekwenda vizuri akiwa na Gerrard ambaye hakuwa na kipaji kama yeye na mara kwa mara alizungumzia vibaya,” alisema Diouf.

No comments