FC BARCELONA YATEUA MKURUGENZI MKUU MPYA KUCHUKUA MIKOBA YA NACHO MESTRE

KLABU ya Barcelona imemteua Oscar Grau kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa klabu hiyo.

Staa huyo wa zamani wa Barcelona ambaye mara kadhaa amekuwa kiongozi katika shule ya watoto aliteuliwa juzi ili aweze kuchukua nafasi ya Nacho Mestre ambaye alikuwa akishikilia wadhifa huo kwenye klabu hiyo ya Camp Nou.

“Bodi ya wakurugenzi imemteua Oscar Grau kuwa mkurugenzi mkuu mtendaji wa FC Barcelona baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Nacho Mestre kumuomba rais apewe muda wa kushughulikia masuala yake binafsi,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo.


“Grau ambaye alikuwa kiongozi mkuu ataendelea kuwa mkurugenzi wa shule ya soka ya FCBE scola. Mabadiliko haya yatatangazwa hivi karibuni,” iliongeza taarifa hiyo.

No comments