Gary Neville amewataka Paul Pogba na Ander Herrera kuthibitisha thamani yao kwa Manchester United dhidi ya mechi kubwa.
Beki huyo wa zamani wa Manchester United ameyasema hayo baada ya viungo hao kung’ara dhidi ya Leicester City Jumamosi iliyopita.
Hata hivyo nyota hao bado hawajaonyesha makali yao ambapo walikuwa chini ya kiwango kwenye mchezo uliowakutanisha na Manchester City na kulala 2-1.

Paul Pogba (katikati) na Ander Herrera (kushoto) walitakata vilivyo dhidi ya Leicester City

Gary Neville (kushoto) anaamini Pobga na Hereira bado hawajaonyesha makali yao kwenye mechi kubwa

Pogba bado ana deni kwa Gary Neville