GK ASEMA MWANAMUZIKI WA KWELI NI YULE ANAYEWEZA “KUBADILIKA”

RAPA mkongwe, King Crazy GK ambaye kwa sasa ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la “Mzuri Pesa”, amefunguka na kusema kwamba wasanii wasiotaka mabadiliko katika muziki ama kazi zao, hawana uwezo wa kubadilika.

Msanii huyo aliyepotea miaka mingi kabla ya kuibuka sasa na wimbo huo mpya ambao hajatumia staili yake ya zamani ya rapu, alisema waasisi wa muziki wa Hiphop na hata muziki huo wa Hiphop pia umebadilika kwa vile mwanzo ulikuwa mgumu na sasa mambo yamebadilika hivyo sio vibaya kwa msanii kubadilika.

Alisema kuwa msanii anayeweza kubadilika ni yule mwenye uwezo wa kubadilika na ndio maana yeye ameweza kubadilika kutoka kurapu hadi kuwa mwimbaji kwa vile ana uwezo wa kubadilika.


“Maisha yanabadilika, tunaangalia soko pia linataka nini, teknolojia na mambo kila siku yanabadilika. Mwanamuziki ni sawa na mwogeleaji au mcheza mpira, muziki hauna kikomo, unaweza kufanya chochote,” alisema GK.

No comments