HARMONISE AFICHUA MASTER J ALIMCHANA SIJUI KUIMBA KWENYE SHINDANO LA BSS

MKALI wa Wimbo “Bado” Harmonize amefunguka kwa kuelezea harakati zake za muziki mpaka anafikia kwenye mafanikio, huku akiweka wazi jinsi alivyoambiwa hajui kuimba na Master J katika shindano la BSS.

Mwimbaji huyo ambaye alishiriki shindano la BSS mwaka 2012 na Walter Chilambo kuondoka na taji hilo, alijiangalia na akajikuta ni kweli alikuwa hajui kuimba.

“Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutokubaliana na matokeo, the way nilivyokuwa naimba kwenye BSS hata mimi ningekuwa ni jaji ningesema wewe huwezi Walter Chilabmo anaweza," alisema Harmonize.

“Sikupaniki kwa sababu toka nikiwa nje Master aliniambia tangu ukiwa nje nilikwambia no, kwa hiyo Master J alinichana kabisa sijui kuimba.” 

Mwimbaji huyo alisema kauli hiyo haikumkatisha tamaa kwani alienderea kupambana kakutafuta njia ya kutokea.

No comments