HARMONIZE AELEZA ALIVYOWAHI KUWA DEREVA WA BODABODA

MSANII wa Bongofleva  kutoka WCB, Harmonize ameeleza jinsi alivyokuwa akichakarika kutafuta maisha kabla ya kujitosa kwenye muziki wa kizazi kipya ambao sasa umemfanya awe maarufu.

Harmonize alikiambia kipindi cha Ngaz’ kwa Ngaz’ kinachoruka kupitia EATV kwamba amewahi kuwa dereva wa bodaboda wakati akiwa kwenye harakati za kusaka maisha.

Alisema kuwa anaiheshimu kazi ya kuendesha bodaboda ambayo anaamini kwamba kama asingejikita kwenye muziki na kupata mafanikio aliyonayo sasa, angeendelea kuwa mwendesha bodaboda.

“Mwaka 2011 niliwahi kuwa dereva wa bodaboda na nimeendesha sana pikipiki, kwa hiyo nina uzoefu kwani nilikuwa nikipakiza abilia kujipatia riziki,” alifunguka Harmonaize.


Msanii huyo alikuwa anaeleza jinsi alivyo na uzoefu wa kuendesha hata pikipiki kubwa ya BMW ambayo alikuwa nayo wakati akishuti video ya wimbo wake wa “Bado”.

No comments