Zlatan Ibrahimovic alimpigia simu wakala Mino Raiola na kumwambia namna anavyohitaji kucheza pamoja na Paul Pogba ndani ya Manchester United.
Mshambuliaji huyo alimwambia: ” Usimuhamishe Pobga kwenda popote zaidi ya Manchester United, nitakuvunja miguu”.
Wakala huyo akafanikiwa kukamilisha utashi wa Ibrahimovic kwa kumpeleka Pobga Manchester United katika usajili uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa.

Zlatan Ibrahimovic ameweka wazi namna alivyovutiwa kucheza na Paul Pogba ndani ya Manchester United

Super-agent Mino Raiola ndiye anayewasimamia Ibrahimovic na Pogba

Raiola aliyempeleka Pobga United kwa pauni milioni 100

Ibrahimovic amemwabia Raiola (kushoto) asimwamishe Pogba, akifanya hivyo atamvunja miguu