IDRIS SULTAN AMCHOKONOA ZARI WA DIAMOND PLATNUMZ

KAMA huwezi utani basi jiweke mbali na Idris Sultan kwa kuwa ipo siku unaweza kujikuta ukifanya kitu usichokitarajia.

Mchekeshaji huyo ameandika ujumbe wa utani kwa Diamond na zari kwenye mtandao wake wa Instagram baada ya hivi karibuni kusambaa kwa taarifa kuwa First Lady huyo wa WCB alikuta heleni kwenye chumba cha Diamond ikionekana kuwa alimsaliti na mwanamke mwingine.

“Ndio imeingia na DHL@ Diamond Platnumz anakupitishia hapo maana umepoteza control mambo yanamwagika ovyo, mara heleni ulizisimamia kama kangaroo,” ameandika Idris kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo.


Hakuishia hapo Idris amempongeza Zari the Boss Lady kwa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuweka picha ya heleni kwenye mtandao huo na kuandika ujumbe unaosomeka: “Happy Birth Day@ Zari the Boss Lady”.

No comments