ISHA MASHAUZI ASEMA WANAOMPIGA MADONGO WANAPIGA NGUMI UKUTA


Mwimbaji bora wa kike wa taarab kwa miaka miwili mfululizo, Isha Mashauzi amesema wasanii na wadau wanaohangaika kumpiga madongo wajue wanajisumbua.

Isha amesema wengi wao wamekuwa wakimchokonoa ili awajibu na kisha majina yao yapande chati, lakini yeye kamwe hawezi kuingia kwenye mtego  wa kitoto.

Akizungumza na Saluti5 wiki hii, Isha Mashauzi amedai wanaofanya hivyo ni sawa na wanapiga ngumi ukuta kwani mwisho wa siku watadharaulika na chati zao kushuka badala ya kupanda kama walivyotarajia.

“Kama kuna msanii anadhani ‘bifu’ linapandisha chati basi upeo wake una mushkel,” alisema Isha.

Mkurugenzi huyo wa Mashauzi Classic akafafanua zaidi: “Hata siku moja sijathubutu kutumia jukwaa langu kumnanga msanii au mdau wa taarab, kwasasabu mimi si muumin wa mbinu hizo za kizamani.

“Wakati nimeondoka Jahazi Modern Taarab na kuanzisha Mashauzi Classic, sikuitukana Jahazi, sikuimba nyimbo za kuikashifu Jahazi na wala sijafanya mahojiano ya kuishutumu Jahazi.
Wakati nimeondoka Jahazi Modern Taarab na kuanzisha Mashauzi Classic, sikuitukana Jahazi, sikuimba nyimbo za kuikashifu Jahazi na wala sijafanya mahojiano ya kuishutumu Jahazi
Isha Mashauzi

“Kwanini nilifanya hivyo? Ni kwasabu najiamini na sikutaka kuitumia Jahazi kama ngazi ya kupandia juu.
"Siku zote mtu mwenye busara hupata ufumbuzi sahihi kwa kila tatizo, lakini mkosefu wa busara hupata tatizo kwenye kila suluhisho .....I will always stay postive.
"Lakini pia yeyote anayejaribu kukushusha chini basi ujue yeye tayari yuko chini yako ...wajipange sana."

No comments