JACK WILSHERE ASEMA KUREJEA KWENYE UBORA WAKE NDIO DAWA YA "KELELE"

STAA Jack Wilshere amesema kwamba alivyopanga ni kuhakikisha anazima lawama kwa kurejea katika ubora wake katika kipindi atakachokuwa akikipiga kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth baada ya kuondoka Arsenal.

Wilshere alijiungana na Bournemouth kwa mkopo wa muda mrefu dakika za mwisho kbla ya dirisha la usajili halijafungwa baada ya kuambiwa na kocha wake Arsene Wenger kwamba atapata shida ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Emirates kutokana na majeraha yanayomkabili.

Kiungo huyo alisota benchi katika mechi yake ya kwanza ambayo timu yao iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya West Broom iliyopigwa Jumamosi wiki iliyopita lakini anasema kuwa atahakikisha ubora wake katika nyimngine zilizobaki msimu huu.


“Pindi linapoibuka swali kuhusu mimi nafahamu ni la ubora wangu. Lakini nina matumaini naweza kucheza mechi nyingi kadri niwezavyo na kumuonyesha kila mmoja kuwa anakuwa anakosea anapohoji kibarua changu,” alisema staa huyo.

"Lengo langu kubwa na ninachokifahamu ni kupata mechi nyingi kadri iwezekanavyo. na hiki ndicho kilichonileta mimi hapa," aliongeza staa huyo.

No comments