JB ASEMA MAISHA YA KUTEGEMEA KIKI ZA SKENDO HUWAFANYA WASANII KUONEKANA WAHUNI

MSANII wa filamu nchini Jacobo Stephen maarufu kama JB amefunguka na kusema kuwa yeye hawalaumu wasanii ambao wamekuwa wakiendesha maisha yao ya sanaa kwa kutafuta kiki au kufanya skendo.

Amesema kwa upande wake yeye hawezi kufanya hivyo kwani anaamini kuwa maisha ya skendo huwafanya wasanii waonekane wahuni washindwe kuaminiwa na kudha lauliwa na baadhi ya watu.


“Siwalaumu wanaopenda skendo sababu ni maisha yao, ila kwangu mimi najisikia vibaya nikiambiwa nimefanya hiki na hiki. Sijisikii vizuri kutokana na jinsi ambavyo nimelelewa na Mungu alivyoniumba. Sasa jeshini ni uvumilivu na kujitambua, ndivyo tulivyofundishwa nah ii imenisaidia kujenga taswira nzuri mbele za watu.”

No comments