JB: WASANII CHIPUKIZI WAKIWEZESHWA WANAWEZA BILA SHAKA

MWIGIZAJI mkogwe katika tasnia ya filamu nchini Jacob Stephen “JB” amesema ana uhakika kwamba wasanii chipukizi wakiwezeshwa wanaweza.

“Kuna wakati haikuwa rahisi sana kuwaamini wasanii chipukizi kwa ajili ya kuwapa kazi waigize wao bila mimi lakini baada ya kufanya katika filamu nzuri ya “Bado Natafuta” na “Chausiku”, nimeamini kwamba kumbe wakiwezeshwa wanaweza,” alisema JB.

Alisema kuwa sasa anajiandaa kuwashangaza mashabiki mara atakapoachia filamu yake ya “Kalambati Lobo” kutoka katika kampuni ya Jerusalem Film ambayo chipukizi wameitedea haki.


“Ninataka kuwaachia vijana wafanye kazi niwasimamie kwa sababu nimegundua kwamba wakiwezeshwa wanaweza kifanya makubwa na ndio maana nimekuwa nikihimiza umuhumu wa kuibua vipaji vipya,” alisema.

No comments