JOSE MARA AHOJI: WEE JOSE MARA UTAISHA LINI!!?


MWIMBAJI na boss wa Mapacha Music Band ameonyesha ‘jeuri’ ya kujiamini katika fani zake na kusema hajui atakwisha lini.

Akiongea kwenye jukwaa la bendi yake ya Mapacha Jumapili usiku ndani ya Meridian Hotel (Club Masai) Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jose Mara akasema yeye ni Jose Mara mwanamuziki, Jose Mara wa redioni (akimaanisha utangazaji), Jose Mara wa u-MC kwenye harusi na sherehe mbali mbali, Jose Mara mjasiriamali.

“Kote huko nafanya vizuri. Wee Jose Mara utaisha lini?” alihoji mwimbaji huyo mwenye vituko vingi na kusababisha ukumbi mzima kulipuka kwa kicheko.

No comments