Habari

JOSE MOURINHO AMPA ONYO ROONEY …amwambia anapaswa kupigania namba

on

JOSE MOURINHO amempa onyo Wayne Rooney kuwa anapaswa kupigania namba ndani ya kikosi cha kwanza ndani cha Manchester United. 
Rooney, 30, alianzia benchi hadi dakika ya 83  Jumamosi mchana wakati Manchester United ilipoiadhibu Leicester City 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ambapo nafasi yake ilitekwa na Marcus Rashford.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mourinho kumpiga benchi Rooney, lakini hata hivyo Mreno huyo amesema mshambuliaji huyo ataendelea kuwa nahodha wa timu hata kama atasugua benchi.
Mourinho alisema: “Nahodha wangu ni Rooney, awe uwanjani au nyumbani, atendelea kuwa nahodha wangu.
“Wakati mwingine najiskia kama mnavyofikiria nafanya kama vile sijui chochote kuhusu soka, lakini najua sheria za mchezo na napaswa kuanza na wachezaji 11 tu.
“Kwahiyo hadi hapo sheria zitakapobadilishwa, ntaanza na wachezaji 11.”
Mourinho amedai kiwango cha Rooney kimeathirika baada ya kusakamwa na mashabiki wa England kufuatia soka dogo alilocheza kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Slovakia mwezi uliopita katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.
Kocha huyo akafichua kuwa kampiga benchi Rooney kwa sababu kasi yake imekuwa ndogo akicheza kando ya Zlatan Ibrahimovic.
Aliongeza:”Pale mshambuliaji mkuu anapokuwa Zlatan, tunahitaji watu wenye kasi wamzunguke. Katika mchezo wa Leicester kumwacha Rooney nje lilikuwa suluhisho kubwa.”
Wayne Rooney watches the early exchanges unfold from his position on the Manchester United subs' bench
Wayne Rooney akiwa benchi

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *