KWA lugha nyepesi unaweza kusema kuwa awaambia “wanalo” wakati utakapoitafakari kauli ya Jose Mourinho anaposema kwamba uzemne wa wachezaji wake Manchester United ndio chanzo cha kufungwa mabao 2-1 na Manchester City katika mtanange wa Manchester derby uliopigwa juzi kwenye uwanja wa Old Trafford.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu England, vijana hao wa Mourinho walibanwa muda mwingi na vijana wa Pep Guardiola ambao walifanikiwa kupata ushindi wakiwa Old Trafford waishukuru mabao ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na nyota wao, Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho.

Akizungumza mara baada ya mechi hiyo, Mourinho alisema kwamba wakati mwingine wachezaji huwa wanafadhaisha makocha.

“Kipindi cha kwanza walikuwa wazuri zaidi kuliko sisi, kwa ujumla tulianza vibaya mechi,” Mourinh aliambia Sky Sport.

“Tuliianza mechi hii huku baadhi ya wachezaji wakiwa chini ya viwango vya kiakili kiasi cha kuwafanya washindwe kuendana na kasi ya michezo,”aliongeza Mreno huyo.

Alisema kuwa katika mchezo huo wachezaji walitakiwa kuwa wepesi na kucheza kwa njia ambayo huwa wanaitumia.

Alisema kuwa katika mchezo huo, wachezaji wawili ama watatu walicheza kwa kiwango cha chini, jambo ambalo liliigharimu timu.


“Kwa kuwa muwazi, walikuwepo wachezaji wawili au watatu waliocheza chini ya kiwango kipindi cha kwanza na kama mechi ingekuwa inachezwa muda huo na ningelifahamu hilo nisingewapanga,” alisema.
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac