JOSE MOURINHO, HENRIKH WAZINGUANA... Henrikh yuko tayari kusepa Manchester United

UTABIRI wa wengi ulionyesha kuwa kocha Jose Mourinho anaweza kutibuana mapema sana na mshambuliaji wake mtukutu na aliyejaa kiburi, Zlatan Ibrahimovic.

Hata hivyo imekuwa sivyo, Mourinho amekwaruzana na kiungo mshambuliaji wake mpya, Henrikh Mkhitaryan aliyemsajili kwa mbwembwe katika usajili wa kiangazi.

Hata hivyo mchezaji huyo ameelezea kukerwa kwa jinsi ambavyo Mourinho anamlazimisha kucheza kama winga ndani ya kikosi cha Manchester United.
Uamuzi huo umemkera Mkhitaryan ambaye amesema kama vipi yuko tayari kuondoka Manchester United licha ya kwamba bado hajalipa deni kwa mashabiki wa klabu hiyo.


Mkhitaryan anayetokea Armenia alisema matarajio ya kucheza kwa furaha Old Trafford yametoweka katokana na uamuzi wa Mourinho ambaye anafanya mambo yake kinyume cha makubaliano yao.

No comments