KAJALA AWATAKA WASANII WENZAKE WAJIONGEZE NA KUJIWEKEA MALENGO

KAJALA Masanja amefunguka na kuwataka wasanii wenzake kujiongeza kwa kufanya mambo kwa ajili ya maisha yao ya baadaye vinginevyo watajikuta wameezeka bila kuwa na chochote walichovuna katika fani hiyo.

Alisema kuwa ametambua hilo kutokana na hali halisi ya jinsi filamu za Tanzania zinavyokosa mvuto tofauti na wakati ule alipoingia kwenye Bongomovies ikiwa na mashabiki wengi.


“Ninasema hivyo kwa sababu hata mimi mwenyewe ninaona kabisa kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda hata mvuto wa kucheza kama mwanamke mrembo unapotea hivyo nimeona niwatadhalishe wenzangu,” alisema Kajala.

No comments