SUPASTAA wa Bollywood mwanamama Katrina Kaif ametwaa tuzo ya Smita Patil Memorial Award inayotolewa na Global Wards ambayo ilitolewa mapema wiki hii.

Katrina ametwaa tuzo hiyo kutokana na kutoa mchango mkubwa kwa jamii kupitia kazi zake za filamu tangu alipojiunga na medani ya filamu miaka zaidi ya 15 sasa.

“Taasisi yetu imempa tuzo ya umahiri katika kuitumikia jamii hasa vijana, msanii Katrina Kaif Septemba 19, mwaka huu, katika hafla iliyohudhuriwa na wasanii na viongozi wa mji,”alisema mwenyekiti wa taasisi hiyo Niranjani Hiranandani.


Alisema kuwa mbali ya tuzo hiyo, pia kuna wasanii kadhaa na watu mbalimbali waliopewa tuzo mbalimbali kutokana na michango yao.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac